Ticker News

Your Ad Spot

Tuesday, September 9, 2025

WAFUGAJI IGUNGA WAKAA MGUU SAWA KUMLAKI RAIS SAMIA

 


Jamii ya wafugaji wa wilayani Igunga mkoani Tabora inasuburi kwa hamu ujio wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa tiketi ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan, anayetarajiwa kuwasili kesho Septemba Septemba 10 na kwa ajili ya Mkutano mkubwa wakampeni.  


Wakizungumza kwenye Mkutano wa maandalizi iliofanyika kata ya  Lububu, mbele ya Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Mrida Mshota, Wafugaji hao walisema kuwa wapo tayari na wamejawa na shauku kubwa kumlaki na kumsikiliza mgombea wa CCM anayetarajiwa kuhutubia na kuomba kura  kwenye viwanja vya Sokonine mjini Igunga. 



" Rais Samia ametufanyia mambo makubwa ya kimaendeleo Sisi wafugaji ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya mifugo yetu kwenye soko, hivyo tuna kila sababu ya kumpokea na kumpigia kura ya ndiyo ifikapo Octoba 29." Anaeleza Kissa Mahona, mfugaji kutoka kijiji cha Chagana katanj Lububu wilayani hapa. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCWT, Mrida Mshota, amesema kuwa, jamii ya kifugaji kote nchini, imefutahishwa mno na uongozi wa awamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu hasani kwa kuwa umeonesha kujali na kushughulikia changamoto zilizokuwa zikiwakabili wafugaji. 



" Wafugaji wanapata mikopo kwenye taasisi za kifedha, wametengewa maeneo ya malisho, soko la mazao ya mifuko lina bei yenye tija,hayo yote n mengine mengi ni juhudi kubwa za Rais Samia."


Mshota amesema kuwa wafugaji hawana cha kumlipa Rais Samia zaidi ya kumpa kura za kishindo ifikapo Octoba 29 ili aendeleze mazuri aloyafanya kwa jamii ya wafugaji kote nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages